GET /api/v0.1/hansard/entries/1338519/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1338519,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1338519/?format=api",
"text_counter": 104,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaunti ya Mombasa, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Watoto wengi wa kike wamepata mimba za kiholelaholela kwa sababu ya kutumia dawa za kulevya. Wanapochukua dawa hizo, hawawezi kujifahamu na wanafanyiwa mambo mabaya bila wao kujua. Dawa za kulevya zimechangia mimba kwa wanafunzi wachanga kwa sababu hawawezi wakajilinda. Watoto na vijana wengi wanaambukizwa maradhi ya zinaa kwa sababu wanatumia sindano sawa. Hakuna kitu kinachowazuia wakiwa wamelewa. Wenyewe wanasema wako high na wengine wanasema, “ arosto noma” . Wakati wanapopata ile arosto, wanasisimuka na kila mtu anakimbilia ile sindano moja ambayo mwenzake ametumia ilhali hajui mwenzake ana maradhi gani."
}