GET /api/v0.1/hansard/entries/1338558/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1338558,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1338558/?format=api",
"text_counter": 143,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Hon. Ali Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Dakika ni moja, kwa hivyo, sitakua na mengi ya kusema ila kumpongeza Mhe. John Makali kwa kupendekeza kuwe na vituo vya matibabu vingi zaidi nchini Kenya. Pia, kando na kuwa na hivyo vituo, ningependekeza vituo hivyo vijengwe nje ya miji ndio vituo hivyo viwe karibu na wananchi. Kama Nyali, kwa mfano, tuko na kituo kimoja karibu na shule ya Frere, ambacho badala ya kusaidia, kinafanya watoto wengi wajiingize kwenye janga la matumizi ya madawa ya kulevya. Isiwe tu dawa za kulevya zinazozungumziwa kila siku bali pia matumizi ya pombe haramu. Dawa za kulevya za heroine na cocaine zimewamaliza watoto wetu katika ukanda wa Pwani. Kwa hivyo, hizo pia zipewe kipau mbele. Ninakubaliana na kauli mbiu ya Mhe. hapa aliposema adhabu ya kifo itolewe. Ukiende mataifa kama Singapore na Malaysia, ukifika katika uwanja wa kimataifa wa ndegeā¦"
}