GET /api/v0.1/hansard/entries/1338618/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1338618,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1338618/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe Spika wa Muda. Ninaunga mkono Hoja ya Mhe. Salasya. Hoja hii ni nzuri sana hasa kwa wakulima wa sukari ambao hupata mapato madogo sana. Wakulima hawa hulima mashamba makubwa lakini mapato yao ni duni sana. Hapo awali, nilikuwa mkulima wa sukari lakini nikakata tamaa kwa sababu ya mapato duni sana kinyume na nilivyokadiria. Hapo nilielewa zaidi jinsi wakulima wa sukari wanapata mtihani. Kumekuwa na tetesi nyingi katika sekta hii ya sukari. Vile vile, zile karatasi za sukari ambazo zimeandikwa, kwa mfano kampuni ya sukari ya Mumias na zinginezo, kumbe waliochapisha ni wale wanaobuni wakijaribu kuchukua nembo za wenzao ili wauze zaidi. Kwa hivyo, Hoja hii ikifaulu, wale wakulima watapata ulinzi katika mazao yao na wauze chapisho zao wenyewe bila kuingiliwa na mtu yeyote. Hawa wakulima wa sukari ndio maskini katika taifa hili ilhali kuna watu wanaoagiza sukari kutoka nchi za nje kama nchi ya Brazil. Sukari nyingine iliingia nchini ikiwa imechafuliwa na zebaki na madhara yake ni magonjwa katika taifa letu. Hoja hii itasaidia kuzuia wale wezi ambao wanatumia njia kama hizi kuleta sukari kutoka nje na kuumiza wakulima wetu. Kwa sababu wengine pia wanataka kuchangia, nitakomea hapa. Ninaunga mkono na kuafiki Hoja hii. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}