GET /api/v0.1/hansard/entries/1338623/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1338623,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1338623/?format=api",
"text_counter": 208,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Nilikua ninataka kuzungumzia kuhusu mihadarati kwa sababu imeniathiri sana katika eneo Bunge la Kisauni lakini sikupata nafasi. Si neno lakini wacha nizungumzie sukari vile imezungumzwa na Mhe. Salasya. Ningependa kusema kwamba Serikali iwe angalifu kwa kulinda viwanda vyetu. Ikiwa viwanda vyetu vinatoa bidhaa ya kutosha, hakuna haja ya kuagiza kutoka mataifa ya nje. Mnapoagiza kutoka mataifa ya nje, mnafanya vijana wetu wengi wakae bila ajira. Ni vyema sana tuvikuze viwanda vyetu ndio tuwe na ajira na nguvu ya kiuchumi ya nchi yetu kindani. Wakulima wetu wanalima sukari na bidhaa zingine, lakini wanashindwa mahali pa kuuzia kwa sababu vitu vingi vingi vimeagizwa kutoka nje. Serikali ikae imara kuhakikisha kwamba tunawapa nguvu wakulima wetu na kuwapa mbolea na kufanya mambo yao yawe rahisi ili wakuze bidhaa nyingi iweze kututosheleza sisi kama taifa. Ikiwa taifa litabidi liagize kutoka nje, ni lazima liweke mikakati kwamba wale watakaoleta sukari kutoka nje, wanaweka vibandiko vyao wao ili wasije wakatumia vyetu ili mnunuzi akienda supermarket ama duka lolote, anafanya maamuzi kwamba sisi tunanunua sukari hii na hii hatutanunua. Kama unavyojua, sukari yetu ya Kenya ni ya Mumias na zingine na ni sukari nzuri na ziko katika uangalifu. Lakini wao wanapoleta sukari, wanaingiza vibandiko hivyo na kututatiza. Ndio maana unaskia kumepatikana sukari ya sumu na mambo haya na yale, kwa sababu tunaruhusu na kuwa rahisi kuwa dumping ground . Watu ni kuja kutupa bidhaa zao. Mimi pia ninaunga mkono kwamba Serikali iweke mikakati mizuri ya kulinda viwanda vyetu ambavyo vinaleta faida. Haina haja ya kuviondoa ama kuleta watu kutoka nje. Kama saa hizi tunakataa ubinafsishwaji wa bandari. Kwa haya mengi, ninasema asante."
}