GET /api/v0.1/hansard/entries/133978/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 133978,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/133978/?format=api",
"text_counter": 457,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Wizara hii. Ninasema hivi kwa sababu kile kinachouma zaidi miongoni mwa wafanyikazi ni kukosekana kwa mapato ya maana. Wafanyikazi nchini wameitegemea Wizara hii miaka nenda, miaka rudi, iyachangie mahitaji yao. Kinachouma zaidi ni kwamba kufikia sasa tumeshuhudia kufanyika kwa migomo ya kila aina siyo kwenye sekta ya kibinafsi peke yake bali pia katika sekta ya umma. Kuanzia kwenye vyuo vyetu vya elimu, imekuwa ni lazima wakufunzi katika vyuo vikuu wagome ndipo waweze kusikika wakidai nyongeza za mishahara. Hilo ni jambo ambalo halifai. Kwa hivyo, inafaa Wizara hii iamue bila ya kupoteza wakati kwamba wananchi wote wa Kenya ni sawa, bila ya kujali aliye juu na aliye chini. Ni jukumu la Wizara hii kuona kwamba imerahisisha kusikizwa kwa kilio cha Wakenya. Hatuwezi kuwa na nchi ambayo ina mwananchi anayelipwa mshahara wa Ksh3.5 million kwa mwezi na mwingine anayelipwa Ksh5,000 kwa mwezi. Katika masoko ya vyakula, na haswa wakati huu wa shida, hakuna soko la mtu anayelipwa Ksh5,000 kwa mwezi na soko la mtu anayelipwa Ksh3.5 million. Ni jukumu la Wizara hii kuona kwamba imeweka viwango vya mishahara ambavyo havina tofauti kubwa sana. Wale wanaolipwa mishahara ya Ksh5,000 kwa mwezi ni wazazi. Kama ni mwanamume, yuko na familia yake. Yuko na watoto ambao wanahitaji kwenda shuleni. Juzi, wafanyakazi wa shirika letu la ndege waligoma. Hata mimi nilisikitika sana kusikia kwamba katika shirika hilo, kuna mtu ambaye analipwa mshahara wa Ksh1.5 million na mwingine ambaye analipwa Ksh8,000 kwa mwezi. Tukiwa taifa, ili Wizara hii kuonekana kwamba inafanya kazi, ni lazima izingatie suala la kuweko kwa mpangilio unaofaa wa mishahara ya wananchi wetu, wawe ni wafinyikazi wa shambani, wafagiaji au askari. Inawezekanaje kwamba tukiwa hapa, tunaongea juu ya ulaji rushwa na magendo halafu askari anayefanya kazi katika kitengo chetu cha kuangalia masuala ya rushwa analipwa Ksh7,500, huku anayemsimamia askari huyo analipwa Ksh700,000? Askari huyo anayelipwa Ksh7,500 ndiye anayetumwa kwenda kuwachunguza wezi. Mwizi anajua kwamba yule mtu anayakwenda kumchunguza ana njaa. Askari anapofika kwa mwizi huyo, kitu cha kwanza ambacho mwizi anafanya ni kumpa askari pesa za kwenda kula. Askari huyo analipwa mshahara wa Ksh7,500, na ameenda kuchunguza mtu aliyeiba Ksh20 million, kisha anapewa Ksh50,000! Kwa hivyo, Wizara hii inafaa kuona kwamba mambo haya ya mishahara yamerekebishwa kabla ya wafanyakazi kutoa fujo na kugoma. Ni haki ya wanafanya kazi wote kupata mishahara mizuri. Wananchi wanajua kwamba sisi hupata mishahara mikubwa. Wao hulipa kodi ili tupate mishahara hii. Ni jukumu ya Wizara hii kuhakikisha ya kwamba matatizo yote ya mishahara yanatatuliwa ili tuepukane na migomo."
}