GET /api/v0.1/hansard/entries/133979/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 133979,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/133979/?format=api",
    "text_counter": 458,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Naibu Spika, watu wetu wanaajiriwa kufanya kazi katika mataifa ya kigeni. Baadhi yao huwa watumwa katika mataifa hayo. Ni juu ya Wizara hii kuhakikisha ya kwamba watu ambao wanakwenda kufanya kazi katika mataifa hayo wanapiga sahihi mikataba kabla ya kuajiriwa. Ni aibu kwa baadhi ya Wakenya kuwa wanafanywa watumwa na Serikali yetu inanyamaza bila kuwatetea. Ni lazima kuwe na mikataba ya kulinda haki zao. Ningehimiza Serikali kuwa na mikataba na nchi za kigeni kabla watu wetu kusafiri kutafuta kazi."
}