GET /api/v0.1/hansard/entries/1340598/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1340598,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1340598/?format=api",
    "text_counter": 154,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa muda. Nachukua nafasi hii kuzungumzia Hoja ya leo. Ni dhahiri shahiri kuwa watoto wengi wako nyumbani, hasa wale wako katika shule za chekechea na msingi. Wazazi wamekuwa na mtihani katika kukidhi matakwa yao katika shule. Katika sheria za Kenya, elimu ni bure katika shule za chekechea, msingi na kwenda mbele. Hoja hii ni nzuri sana, tukizingatia kuwa tunataka Serikali iongeze ruzuku ya watoto katika shule. Watoto wengi katika shule za msingi wamekuwa chokoraa kule barabarani. Pengine akienda shule, anaulizwa remedial fee. Anapoambiwa aende akanunue kitu fulani, mzazi hawezi nunua. Iwapo tunaweza kuongeza ruzuku au capitation shuleni, wazazi watakuwa na wepesi wa kupeleka watoto shule na tutaweza kupigana na ndoa za mapema. Katika NG-CDF na National Government Affirmative Action Fund (NGAAF), tunashughulika kulipa masomo ya shule ya upili na colleges. Elimu huanza chini. Ili uweze kumpatia mtoto msingi mzuri wa elimu, lazima apate chakula kizuri na awe darasani kila wakati. Mtoto akitoka nyumbani kama tumbo halina chochote, lazima apate kitu akifika shuleni. Mhe. Spika wa Muda, lazima mtoto akitoka nyumbani hata kama tumbo likiwa halina chochote akifika skuli apate riziki ndio aweze kuwa makini kwa masomo yake. Katika Gatuzi letu la Mombasa, ukienda ndani kwenye jiji, utapata watoto wengi wamekuwa omba-omba barabarani. Kwa sababu gani? Wazazi tumeacha kufuatilia. Serikali imeweka elimu ya bure, lakini haifuatiliwi na kuzingatiwa vizuri. Watoto wakipelekwa skuli wanaitishwa mambo mengi sana. Na mara utapata yuko barabarani. Ukiwauliza wanakuambia walifukuzwa wakalete vitabu au vitu fulani. Naiomba Serikali kuwa kama tuliweka elimu ya bure, tuzingatie mtoto akifika shuleni."
}