GET /api/v0.1/hansard/entries/1340600/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1340600,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1340600/?format=api",
    "text_counter": 156,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "sheria ya elimu iwe ya bure. Lakini wanafunzi wakifika skuli, wanaulizwa mambo mengi sana. Na ndio maana mimi ninaomba zile pesa za wanafunzi zinazopewa na Serikali ziongezewe. Ama wasindize ile misaada ili iweze kwenda shuleni ili wanafunzi wasome bila kufukuzwa na kuulizwa mambo mengi. Katika kaunti yangu, watoto wamepata mimba za mapema. Wanafunzi wa shule za msingi wanahitaji sodo, na kuangaliwa vizuri. Bila sodo, utapata wamerudi nyumbani. Wanakutana na mtu barabarani anawaambia nitakupa mia au mia mbili na anawaambia: “Njoo tupite kwa kando nikufanye hivi na vile.” Mwishowe, mtoto anapata uja uzito na hawezi kuendelea tena na masomo. Tunaona mimba za mapema zinaendelea kukithiri katika kaunti ama taifa letu. Sisi tunauliza sodo ziko wapi? Ninauliza kama Mama Kaunti. Tumetolewa bajeti ya kupeleka sodo katika skuli lakini mpaka leo hatujapata. Watoto wanahangaika katika masomo yao. Kwa hivyo, ninaunga Mjadala huu mkono, isipokuwa ninasema iko katika Katiba na iweze tu kufuatwa, kusisitizwa na kutiliwa mkazo Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}