GET /api/v0.1/hansard/entries/1340620/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1340620,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1340620/?format=api",
    "text_counter": 176,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Magarini, ODM",
    "speaker_title": "Harrison Kombe",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Mhe. Wakili Muriu ana mipango mizuri kwa watoto wa Kenya, lakini hicho kipengele kwamba NG- CDF isimamie elimu ya msingi ni kinyume cha Katiba. Hapo amekiuka Katiba maana elimu ya msingi ni bure, na ni ya lazima. Tukisema ni bure na ni ya lazima, haimaanishi kwamba haigharamiwi. Bali ni Serikali inagharamia hiyo elimu ya msingi. Mhe. Wakili anastahili kuwakilisha haki, lakini yeye mwenyewe anakiuka Katiba na kugeuka mgandamizi wa haki kwa wale wa elimu ya juu. Kile ambacho binafsi ningeunga mkono ni kama angesema kwamba zile hela zimetengewa elimu ya msingi ziongezwe kwa asilimia mia moja. Hilo lingekuwa ni jambo la busara, na tungeliunga mkono. Zaidi, serikali ingeongeza hiyo ruzuku kwa hiyo elimu ambayo inastahili kuwa ya bure na ya lazima. Ahsante, Mhe. Spika wa Muda."
}