GET /api/v0.1/hansard/entries/1340642/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1340642,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1340642/?format=api",
"text_counter": 198,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuchangia Hoja hii. Kwanza, ninampongeza Mhe. Wakili Edward Muriu kwa kuwaza na kuleta Hoja hii hapa ili tuweze kuijadili. Ninaiunga mkono. Ni vyema tuwe na mipango ya kuongezea pesa kwa mfumo huu wa NG-CDF ili maswala ya kupata lishe shuleni yaweze kuangaziwa. Wengine wetu hapa tumesoma kupitia changamoto nyingi sana. Motisha iliyokuwa inatupeleka shuleni ni ya yale maziwa ya nyayo. Wakati mwingine, huo tu ndio uliokuwa mlo tuliopata kwa siku. Kwa hivyo, ninaunga mkono kabisa swala la kuwepo kwa chakula shuleni ili wanafunzi wapate hata kama ni mlo mmoja kwa siku. Sasa hivi, familia nyingi zinakumbwa na changamoto nyingi za kifedha. Kuna watoto wengi wanaolala bila hata mlo mmoja kwa siku. Kwa hivyo, kuwepo kwa chakula hiki shuleni kutawavutia watoto kuenda shule. Vile vile, tunajua kuwa mpangilio huu ukiafikiwa… Mhe. Muriu, usiwachie Hoja hii hapo tu, bali ipeleke mbele kabisa ili iwe sheria tunayoweza kufanikisha. Tunaomba mlo huo uwe ni safi, kwa wakati sawa, na uwe ni lishe bora, yaani balanced diet. Ahsante sana. Ninaunga mkono."
}