GET /api/v0.1/hansard/entries/1340670/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1340670,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1340670/?format=api",
    "text_counter": 226,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Wabunge wengi wanakimbilia mashirika ya kibinafsi kama vile Tap2Eat ambayo inawasiliana na NG-CDF kujenga meko ya kisasa ili chakula kipatikane katika shule za msingi. Uhusiano huo umetokana na matatizo ya Wabunge kutoweza kufika katika shule za msingi. Kipengele cha 53(1)(b) cha Katiba ya Kenya kinasema kuwa kila mtoto ana haki ya elimu. Kipengele cha 53(1)(c) kinaongea kuhusu lishe bora na kuhakikisha kuwa watoto wana afya bora."
}