GET /api/v0.1/hansard/entries/1340712/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1340712,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1340712/?format=api",
    "text_counter": 268,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": "Katika sehemu ambazo tunaishi, utapata kuna sehemu zinaitwa Wines and Spirits . Utapata mtu ametengeneza kibanda ambacho anauza pombe kali sana. Pombe hizo zimetiwa katika vipakiti vidogo vidogo na huuzwa kwa bei rahisi sana. Inawezekana hata mtoto wa shule akazinunua kwa shilingi hamsini na kuzitumia. Wakati mwafaka umefika. Ni lazima pia tupige msasa, kupitia serikali za kaunti, suala hili. Ni lazima tuhakikishe kwamba wanaangalia sehemu ambazo biashara kama hizi zinawekwa. Wakati umefika hospitali zetu ziwe na sehemu ambazo zitakuwa zinazungumzia mambo ya madawa ya kulevya na pombe haramu ili tuweze kunasua Wakenya wetu wengi ambao wameingia katika mitihani kama hii na kuharibu maisha yao."
}