GET /api/v0.1/hansard/entries/1340713/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1340713,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1340713/?format=api",
"text_counter": 269,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "Wakati wa nyuma, tulikuwa na maafisa ambao walikuwa wanatembea nyanjani wakizungumzia mambo ya kupanga uzazi, maradhi ya HIV, kilimo na mengineyo. Wakati umefika tuwe na maofisa wakutembea nyanjani na maskani ambayo vijana hawa wanafanya shughuli nyingi sana za mihadarati, kunywa pombe na mambo kama hayo. Umma wetu unapotea. Watoto wetu wadogo sana, miaka kumi na minane kuja chini, hata miaka kumi na mitano kuja chini, wameingia katika matumizi ya mihadarati na pombe haramu. Hatuna umma ule mchanga ambao utaweza kufikiria mambo ya maisha na kujenga uchumi kwa sababu wameingia katika mambo haya."
}