GET /api/v0.1/hansard/entries/1340716/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1340716,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1340716/?format=api",
"text_counter": 272,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "(ACC), mpaka kwa polisi wetu, je, wamechukua mikakati ipi kuhakikisha kwamba madawa ya kulevya hayaingii hapa nchini? Haya madawa ya kulevya hayapaswi kufika kule nyanjani. Hii ni kwa sababu, wakati madawa haya hayakuwa yanafika nyanjani, hatukuwa na takwimu kubwa za kuonyesha kwamba vijana wamebobea katika mambo haya. Lakini kwa sababu ni rahisi kupata mihadarati na pombe haramu, kila mmoja ameingia katika matumuzi yake. Hivyo basi, uchumi unadorora na maisha na afya ya Wakenya inadorora. Ni wakati mwafaka Serikali iangalie vile inavyofadhili NACADA. NACADA ni taasisi, lakini ufadhili wake ni mchache sana. Katika mipaka yetu, hakuna maofisa wa NACADA wa kuhakikisha kwamba mihadarati haipitii hapo na kufika huku nyanjani. Kule Busia, Malaba, na Lunga Lunga, mihadarati inapita kwa njia nyingi sana. Mihadarati pia hupitia baharini. Ni wakati mwafaka kuwe na vitengo vya usalama mahsusi ambavyo vimewekwa kuangalia suala la mihadarati."
}