GET /api/v0.1/hansard/entries/1340760/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1340760,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1340760/?format=api",
    "text_counter": 30,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
    "speaker": null,
    "content": " Ninashukuru kwa fursa hii, Mhe. Spika wa Muda. Ninataka kuongeza sauti yangu kwa kujadili suala hili kwa ufupi kwa kuwa limekuwa donda sugu. Tuko na mbuga ya wanyama karibu na sisi huko Taita/Taveta. Mara nyingi, wanyama huvuka na kuchanganyika na watu. Tumeshuhudia wanyama wakiua watu na kuharibu mimea. Wakati wa janga kama vile ukame ulioko sasa, wafugaji hukosa kabisa mahali pa kulisha wanyama. Kwa kweli, KWS hawashirikiani na majirani wake kabisa, haswa wakaazi wa Taita/Taveta. Zaidi ni pale Taveta ambapo Mhe. Bwire amezungumzia. Tumeona mifugo ya watu wengine wakilishwa mbugani na hakuna hatua yoyote imechukuliwa. Lakini, hawa majirani wa mbuga ya wanyama ya Tsavo walioko pale Taveta wanahangaishwa. Wamepata shida nyingi huku wakihangaishwa kwa kushikwa na kutendewa kila aina ya ufedhuli. Wanashikwa na hawaambiwi watalipa faini kiasi gani. Imekuwa shida kubwa kwani wao hushikwa na mifugo wao kuzuiliwa."
}