GET /api/v0.1/hansard/entries/1340761/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1340761,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1340761/?format=api",
"text_counter": 31,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
"speaker": null,
"content": "Sisi kama viongozi tumepata shida. Hakuna ushirikiano wowote tukijaribu kuzungumza nao. Ninamshukuru Mhe. Bwire kwa kuleta Ombi hili Bungeni. Ninaomba tusaidike kwa sababu ujirani mwema ni kufaana. Tunaumia kila wakati wanyama wakivuka. Tunadhulumiwa. Tumekuwa na changamoto nyingi hasa ukosefu wa chakula cha mifugo. Hata kama mifugo watapita na kuingia kwenye National Park, basi sheria ifuatwe. Haipaswi kushika watu na kuwazuia bila hata faini."
}