GET /api/v0.1/hansard/entries/1340777/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1340777,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1340777/?format=api",
    "text_counter": 47,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Gertrude Mwanyanje",
    "speaker": null,
    "content": " Asante Mhe. Spika wa Muda. Ninataka kuzungumzia ardhilhali hii na kuunga mkono Mhe. Bwire kutoka Taveta. Hii ni kwa sababu Taveta inapakana na Jimbo la Kilifi upande wa Ganze na Bamba ambako hakuna mavuno na chakula kwa sababu ya wanyama pori. Kule Palakumi, Jaribuni na Mayowe utapata fisi wanaingia kwenye maboma ya watu na kula mifugo. Ndovu, kule Bamba na Ganze, huharibu na kula mimea yote. Saa hizi watu wetu hawana chakula. Tumekuwa na mvua nzuri sana ya kukuza mazao lakini wanyama pori kutoka Tsavo Mashariki wameingia Kilifi kupitia Bamba na Ganze na kutuharibia mazao yetu. Jambo la kusikitisha ni kwamba maofisa wa wanyama pori ni wavivu; hawasikizi na hawashiki simu wakipigiwa kuambiwa kwamba ndovu wameonekana na wanaharibu mimea. Hawajali na hawatoki mpaka wanyama wamalize kuharibu mimea. Saa hizi tunalia na wananchi. Ombi langu kupitia hili Jumba ni kwamba watu wetu waweze kulipwa fidia. Wakulima wote ambao mifugo wao imeliwa na kutobolewa na fisi... Saa hizi hakuna mifugo kule Mayowe wala kule Bamba na Vitengeni. Aidha hakuna mimea kwa sababu ya ndovu wanaotoka kule Taveta, Tsavo Mashariki. Tunataka kuona ni vipi hawa maofisa wa misitu…"
}