GET /api/v0.1/hansard/entries/1340780/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1340780,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1340780/?format=api",
    "text_counter": 50,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Molo, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Kuria Kimani",
    "speaker": null,
    "content": "wazee wao walikuwa wanaenda nyumbani mapema kwa kuogopa kupatikana na yule ndovu. Sasa hatari imezidi hadi wanasema afadhali wazee wachelewe kidogo na huyu ndovu aondolewe kabisa katika maeneo hayo. Saa zingine wananiambia niwapatie nafasi wakabiliane na huyo ndovu. Lakini nimewaambia wakikabiliana naye, basi watashikwa na askari na kujipata matatani kisheria. Kwa hivyo, ninawaomba wakati mnaangalia hii ardhilhali, mkumbuke wananchi wa Soin na Sachangwan ambao wanasumbuliwa na ndovu. Wamempatia jina la David. Tafadhali, wana KWS kujeni mchukue David wenu maana tumechoka kwenda nyumbani mapema. Asante sana Mhe. Naibu Spika."
}