GET /api/v0.1/hansard/entries/1341367/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1341367,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1341367/?format=api",
    "text_counter": 637,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ahsante, Mheshimiwa Spika wa Muda. Kwanza, nachukua nafasi hii kumpongeza ndugu yangu, Mheshimiwa Gikaria, kwa kuleta Mswada huu Bungeni. Ni dhahiri kuwa vijana wengi wana matamanio ya kujitegemea. Wangependa kuwa wanakandarasi, lakini zile hela zinazotozwa na zile mikakati za kuwa mwanakandarasi ndizo zinazowalemea vijana wengi. Ninazungumza hivi kwa sababu wakati nilipokuwa nikitafuta kura, niliwaambia vijana wajibidiishe na kubuni makampuni ili wawe wanakandarasi. Wenyewe wafanye kazi itakayopatikana, na ile shilingi watakayopata ibaki hapo mtaani. Mama mboga na mama chapati-maharagwe watapata riziki yao. Kuna mwendo mrefu wa kupata hati ya kuwa mwanakandarasi. Hivyo basi, wapewe hela hizi ili waweze kuanzisha makampuni na kuwa wanakandarasi. Watakapopata kazi baadaye, watazilipa hela hizo. Hakika sitajali hata kama kutakuwa na riba. Itakuwa si neno kwa sababu tayari watakuwa wamepata hizo kandarasi na wakimaliza kazi, wataweza kulipa. Nimesikia mnenaji mmoja akiuliza kwa nini tunawapa vijana nafasi hizi, ilihali hata hawajajistawisha. Hiyo ni sawa na kutangaza kazi na kusema kuwa unatafuta daktari aliye na ujuzi wa miaka kumi. Ikiwa daktari aliye na ujuzi wa miaka kumi hangekuwa ameajiriwa pale mwanzoni, angetoa wapi huo ujuzi wa miaka kumi? Ni lazima kwanza apate hiyo kazi ili aweze kupata hiyo tajriba akiwa kazini. Naunga mkono Mswada huu. Ikifika wakati wa Kamati ya Jumba Lote, tutafanya marekebisho ili kuhakikisha kuwa nafasi hii inayotolewa haitatumika vibaya. Itabidi tuangalie kiwango cha miaka cha vijana wetu, hata kama ni miaka ishirini na mitano kurudi nyuma. Hiyo itawawezesha vijana wetu kusamehewa na kupata hati hizo bila malipo, kisha walipe baadaye. Hiyo itakuwa ni hali nzuri.. Hivyo basi, nakushukuru, Mheshimiwa Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi ya kuuunga mkono Mswada huu."
}