GET /api/v0.1/hansard/entries/1342374/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1342374,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1342374/?format=api",
"text_counter": 273,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nimesimama kuunga mkono Kamati kwa kazi nzuri iliyofanya. Uhuru ulipatikana kote nchini baada ya kubuniwa kwa Halmashauri ya Barabara za Mashambani. Punde tu, ndipo tulipata kuona sehemu zile ambazo hazipitiki zinarekebishwa na hivi sasa tunajivunia kwamba tuna barabara. Mhe. Spika wa Muda, ningeomba na kupendekeza kwamba badala ya kupunguza hela hizi za Halmashauri ya Barabara za Mashambani asilimia 10 iongezwe hadi asilimia 15. Asimilia 22 iongezwe hadi asilimilia 25 na asilimia 32 iongezwe hadi asimilia 35. Hivyo, Kenya nzima itakuwa na barabara za kujivunia huko mashambani. Hivi sasa, matunda na vyakula vingine vinaharibikia mashambani kwa sababu hatuwezi kuvisafirisha hadi soko kwa sababu ya hali mbaya ya barabara tulizonazo. Mhe. Spika wa Muda, ningependa kusema kwamba tusifunike blanketi kaunti zote. Ningependa kuitenganisha Kaunti yangu ya Kilifi kwa sababu kile kidogo wanachopata kinaonekana. Wamejaribu kurekebisha barabara nyingi ijapokuwa Halmashauri ya Barabara za Mashambani imefanya vyema zaidi kuliko hizo kaunti. Sehemu nyingi zimerekebishwa isipokuwa barabara moja kutoka GIS kwenda Ramada. Lakini habari zilizoko ofisini kwangu ni kwamba mwanakandarasi atafika hivi karibuni."
}