GET /api/v0.1/hansard/entries/1346045/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1346045,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1346045/?format=api",
    "text_counter": 110,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii ili kuomboleza mwenda zake Mhe. Lawrence Sifuna ambaye alihudumu kama Mbunge katika Bunge la Kitaifa. Kifo cha mwenda zake Sifuna kimepokonya nchi hii mmoja wa viongozi wa ukombozi wa pili ambao walijitolea kihali na mali kuhakikisha ya kwamba tunapata ukombozi wa pili ambao ulikuwa ni ukombozi ambao sisi zote tunaweza kujivunia. Kujitolea kwake na wale wengine ambao walipigania ukombozi wa pili, akiwemo Baba Raila Amollo Odinga na wengine ni ushahidi wa kutosha ya kwamba wale ambao wamepigania nchi hii, wameweza kuipeleka nchi mbele na kwa sasa tunajivunia demokrasia ambayo tuko nayo katika nchi yetu ya Kenya. Jambo la kusikitisha ni kwamba yale yote ambayo yameweza kupatikana katika ukombozi wa pili, katika hali tuliyo nayo, sasa yote yameanza kudidimia. Tumeona hivi majuzi baadhi ya rasilimali za nchi kama vile Jumba la Mikutano la KICC, Shirika la Kenya Pipeline na zingine zimewekwa kwenye mnada kuuzwa ili inasemekana itasaidia kupunguza madeni ambayo nchi hii iko nayo. Mashirika haya yalipoundwa, kulikuweko na umuhimu na dharura ya kuwa na mashirika kama hayo. Kwa mfano, Kenya Pipeline Corporation ambayo ilianza pale Jomvu, karibu na nyumbani kwetu, ni shirika ambalo limechangia pakubwa kupunguza gharama ya mafuta katika nchi yetu ya Kenya. Hii ni kwa sababu mafuta yanapelekwa na pipeline kutoka Kaunti ya Mombasa mpaka Kaunti ya Nairobi na Western - Eldoret - halafu inafikishwa nchi ambayo ni rahisi zaidi kuliko kutumia magari, kuyatoa Kaunti ya Mombasa mpaka Eldoret. Shirika kama hili lina kazi muhimu ya kuweza kuhakikisha kwamba bei ya mafuta haikurupuki tukashindwa kulipa. Likipelekwa katika mikono ya watu binafsi, itakuwa hasara kwa nchi. Hii ni kwa sababu huduma ambayo shirika hili linatoa ni huduma ambayo ikipeanwa kwa mikono ya kibinafsi, sisi wananchi hatuna uwezo wa kujua kitu gani kinaendelea na zile ambazo zinawekwa pale. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}