GET /api/v0.1/hansard/entries/1346374/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1346374,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1346374/?format=api",
"text_counter": 266,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "tuwe Waafrika wasiotegemea mataifa ya nje. Alikuwa sawa kabisa kwa sababu anajua kwamba wakati mwingine sisi kama Waafrika tunahadaiwa juu ya njaa. Watoto wetu hawana lishe bora na mengine ya kutudhuru yanaingia katika taifa. Itakuwa bora tukiwapa wakulima wetu mbegu, teknolojia nzuri ya kukuza mazao yao shambani, na kuwapa mbolea na nafasi nzuri ya kunyunyizia mimea shambani. Baadaye, tuwawezesha kuweka mavuno ndani ya maghala yao. Tunafaa kuwapa namna ya kuhifadhi chakula katika maghala ili tusiwe na njaa msimu wa kiangazi. Wao watatoa vyakula katika maghala yatakayolisha taifa. Hii ni juhudi nzuri imefanywa na viongozi wa Afrika Mashariki. Huenda Kenya iwe na msimu wa kiangazi wakati fulani ilihali Tanzania ni msimu wa kuvuna. Ni vizuri tukiaminiana vizuri kati ya mataifa ya Afrika ya Mashariki. Kama watu wetu wa Kenya wako katika kiangazi, wao wakivuna sisi tutapata chakula. Chakula kitatoka Kenya kusaidia wengine katika kanda hii. Itakuwa tunasaidiana ili watoto wetu wapate lishe bora. Itakuwa hatutoi ule mwanya wa mtu kuja kutwambia, “Leo mna njaa. Kwa hivyo, mimi nitawapa chakula na ninyi mnipe hiki na kile. Kisha nitatoa deni zenu ili mpate chakula.” Hilo halitatokea. Tukiwa na taifa lililo na chakula na udongo sawa, mambo mengine yote yataenda sawa. Wakati mwingi ule umaskini ndio huchangia Mwafrika kuonekana kama si chochote mbele ya dunia. Viongozi wetu wakishirikiana... Mimi nikiona viongozi wa Afrika Mashariki wamekaa pamoja wakipanga mikakati ya mataifa ya Afrika Mashariki, kama mama kaunti wa Mombasa, husikia vizuri sana. Leo ninampongeza Rais Samia Suluhu kwa juhudi anazofanya kuhakikisha Marais wetu wanakaa kuhakikisha hali inakuwa nzuri. Ninajua huu mkutano ulifanyika katika Taifa la Rwanda. Juzi nimetembelea Rwanda na kuangalia maisha yao yalivyo. Nilisema ni kweli Afrika inaamka. Watoto wa Kiafrika hawawezi kuwa ndio picha za kwashiorkor au marasmus viongozi wetu wakiafikiana tuwe na lishe bora na usalama wa chakula."
}