GET /api/v0.1/hansard/entries/1347433/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1347433,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1347433/?format=api",
"text_counter": 305,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bi. Spika wa Muda, nachukua nafasi hii kumpongeza Kiongozi wa Wengi katika Seneti aliyeleta Mswada huu. Sisi tulilelewa Mombasa ambako kuna hiyo Tea Auction. Tulisoma Chuo Kikuu, tukamaliza na tukaanza kufanya kazi Mombasa. Nilifungua ofisi yangu ya uwakili mjini Mombasa. Kati ya wale watu kila wakili mjini Mombasa alitarajia kufanya kazi nao au kuwa mteja wao, ni wale waliokuwa wanafanya kazi ya Tea Auction . Wale watu ambao walikuwa matajiri, wanaishi vizuri na waliomiliki nyumba katika eneo ya kifahari inayoitwa Nyali miaka ile tulipokuwa watoto, walikuwa wanafanya kazi katika Tea Auction . Hivyo basi, kusikia ya kwamba wale wanaokuza majani chai na wanaofanya kazi wa kuvuna haya majani ni watu wanaishi kwa uchochole na umaskini ni jambo la kusikitisha sana. Jambo ambalo ninalifurahia ni kuwa Serikali hii imeamua haitafanya mabadiliko ya kijuujuu yanayojulikana kwa Kingereza kama cosmetic changes. Hatutafanya hayo kwa sababu hayatasaidia mkulima wa kahawa, mahindi na majani chai. Mkulima wa majani chai anataka kupata haki yake na ndio sababu huu Mswada umeletwa hapa. Tumeambiwa kuna wakati Mswada huu uliletwa mbele ya hii Seneti na pia ukapitishwa na National Assembly . Lakini kuna makosa yaliyokuwepo katika ile sheria iliyopitishwa na ndio maana umeletwa kwa mara ya pili kupigwa msasa."
}