GET /api/v0.1/hansard/entries/1347437/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1347437,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1347437/?format=api",
    "text_counter": 309,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ni nini? Tulikuwa tunasikia Mhe. Rais kwa wale Marais waliotangulia akisema “Wakulima wa kahawa, deni lenu bilioni mbili tunalipa.” Halafu makofi Hoyee! Halafu mwaka unaofuata, tunarudi palepale. “Wakulima wa majani chai, deni lenu la bilioni moja, Serikali hii italipa.” Halafu makofi hoyee! Lakini mwaka unaofuata, uchochole na umaskini unarudi tena. Serikali hii imeamua ya kwamba, ikiwa tunataka kufanya mabadiliko, kwanza tunaangalia sheria iliyopo. Ile sheria tukiirekebisha na kuipiga msasa, itamsaidiaje yule mkulima wa kawaida kule mashinani. Ndio maana nimesimama kidete kusema kwa sauti moja kwamba Mswada hu tuupitishe kama Seneti. Ni Mswada wa kupigwa msasa. Tunaomba Maseneta wote wanaozungumzia huu Mswada tuupige msasa sawasawa. Ninafurahi Sen. Cherarkey amesema wakati wa Mswada huu kusomwa mara ya tatu, ataleta marekebisho mengine. Tunataka Maseneta wengine, hasa wale wanaotoka sehemu inayokuzwa majani chai, wausome Mswada huu, tuupige msasa na tujaribu kuweka vipengele vitakavyosaidia mwananchi wa kawaida. Kwa wananchi wa kawaida wanaonisikiza wakati huu, tunawaomba wajue ukweli wa mambo ni kwamba kuna siasa duni na siasa ya ukweli. Siasa ya ukweli ni kama hii kazi tunayofanya hapa. Siasa duni ni ile ya makofi na kupigiwa kelele na kubebwa juu juu. Ile haibadilishi kitu. Mtu akija na akuambie majani yako ya chai tunalipa deni lako halafu mwaka kesho unarudi kwa deni, hajakusaidia. Mtu akikuambia sheria tunaibadilisha ili uweze kuuza majani yako ya chai kwa bei inayokufaa wewe, ili uweze kupata manufaa katika ukulima wako, huyo mtu ndiye anafanya siasa ya ukweli. Sisi katika Serikali hii, hatutarudi kufanya siasa ya uwongo kwa wananchi hata kama ni ngumu. Ndio sababu wakati mwingine tunapigwa, tunatandikwa kwa mitandao na watu wa upinzani wanasema hii Serikali ni mbaya. Lakini ni sawa. Wacha waseme. Sisi tunafuata mipangilio kwa sababu kugeuza hali ya mwananchi wa kawaida, kuna vipengele vya sheria ambavyo lazima tuvigeuze ili apate haki yake. Kwa hivyo, tukiwa hapa Seneti, tunasema katika huu Mswada, kuna vipengele ambavyo vimewekwa, hasa direct sales . Tumeambiwa kuna Gavana aliyejaribu kwenda kuuza lakini hakufanikiwa. Lakini alisahau kuambia Seneti ya kwamba, sheria iliyokuwepo wakati huo na ambayo lazima tuigeuze, haikuruhusu kuuza moja kwa moja au direct sales. Sasa tunaleta sheria hii inayosema, on average at least for the next three months, yaani miezi mitatu iliyopita, ile bei ikiwa iko juu kidogo, basi unakubaliwa kuuza. Sisi tutafurahia sana kuona hii inaleta faida kwa wananchi wa Kenya. Jambo lingine ambalo tungependa sana lieleweke ni kwamba majani chai ya Kenya yanadhaminiwa sana duniani. Wakati wanatengeneza majani chai mengi na ya aina tofauti tofauti za ladha ya chai, wanatumia majani ya chai ya Kenya. Kwa hivyo, wamegeuza zile ladha zikawa nzuri na kuziuza. Lakini wanapofanya hivyo, Wakenya wakulima waliofanya hiyo kazi, hawapati hiyo faida."
}