GET /api/v0.1/hansard/entries/1347439/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1347439,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1347439/?format=api",
"text_counter": 311,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Unasikia Wazungu walioweka majina yao pale ndio wanaopata ile faida na hawakulima. Ukienda saa hii uzunguni utasikia kuna English tea . Lakini ukiangalia Uingereza ni nchi ya visiwa kadha wa kadha; ni bahari kila mahali. Hakuna ardhi ya kulima majani chai. Sasa, ilikuwaje tena wao wana English tea na hawana ardhi ya kukuza majani chai? Wametutumia vibaya kwa miaka mingi. Tungependa sasa kupitia huu Mswada na wale wenzetu wa Bunge la Kitaifa na Maseneta wenzangu tunaouangalia huu Mswada tuupige msasa ili hata wale wawekezaji wanaokuja kuchukua haya majani ya chai, waweze kuweka viwanda vitakavyo jaribu kuweka dhamani kidogo ili watu wakienda kuuza wasikie ya kwamba ni chai ya Kenya na sio chai wa Wazungu wa Uingereza. Mwingereza hajui hata kuchuna majani chai. Hawajui vile haya mambo hufanywa lakini wamejiweka mbele kwa sababu wao ndio wanaotengeneza haya majani ya chai kwa kuyasaga na kuyageuza kuwa ndio haya tunayokunywa. Hivyo basi, nawaomba Maseneta wenzangu tulioko hapa, tuupitishe Mswada huu kwa roho moja na safi tusaidie wakulima wetu wanaoumia sasa kwa sababu bei ni mbaya na wanaofaidika ni mabwenyenye ambao hawajaona vile wakulima wanasumbuka kuleta majani chai sokoni. Tuliwaona wale matajiri ambao wako katika ile tea auction kule Mombasa. Hatukatai mnafanya kazi yenu, lakini pia angalieni, mkuwe na roho maanake siyo haki wewe unapeleka gari nzuri iliyo na air condition, unaishi maisha mazuri, unakaa nyumba nzuri ya kifahari, una akaunti nono ya benki, lakini yule ambaye anakuletea yale majani yanayokutajirisha wewe na familia yako, ni maskini mchochole na hata mtoto wake haendi shule. Hili siyo jambo nzuri. Lazima waangalie tena namna ambayo mwananchi wa kawaida atapata fedha kwa ile kazi anayoifanya. Bi. Spika wa Muda, mara nyingi tukiwa tunaleta hizi sheria, wale mabwenyenye kule nje wanaziangalia kuona ni kitu gani ambacho tutaweka kama kizingiti ili ile sheria isipite. Wakisikia kuna tea levy, hawataki kulipa. Kwa hivyo, wanaangalia namna ya kuvuruga na kuharibu ili yule mtu wa kawaida asipate na wao waendelee na yale maisha yao. Kwa hivyo, nawaomba wale ambao wataangalia Mswada huu katika Third"
}