GET /api/v0.1/hansard/entries/1347441/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1347441,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1347441/?format=api",
    "text_counter": 313,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": ", tuuangalie kwa makini. Tusiwapatie nafasi hawa mabwenyenye waendelee kuwakandamiza watu wetu. Mimi najua kuna watu wanaisikiza sana majadiliano yetu juu ya Mswada huu wa majani chai na wanayafuatilia kwa macho makali na umakini. Mimi najua, maanake hata asubuhi leo nilipokuwa kortini kwa kesi zingine tunazozifanya, kuna mawakili ambao waliniambia ya kwamba wanajua leo kutakuwa tunaujadili hii Mswada huu na wataisikiliza kwa makini. Mimi najua mabwenyenye washawatuma watu ili waangalie ni namna gani watavuruga. Kwa hivyo, naomba tuifanye kazi yetu kwa makini. Tujaribu sana tuifanye vizuri na tusiwape watu nafasi kuivuruga. Tunataka wananchi wetu walio mashambani waanze kupata haki yao. Ile haki yao ambayo Mwenyezi Mungu anawapatia kupitia kazi wanazofanya mashambani."
}