GET /api/v0.1/hansard/entries/1347756/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1347756,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1347756/?format=api",
    "text_counter": 249,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Pia mimi ningependa kuchukua fursa hii kumpongeza aliyeleta Hoja hii. Ni muhumu sana kubuni kamati ya kitaifa itakayo washughulikia wazee, ambao ni chombo muhimu sana. Katika uzeeni, kuna matatizo mengi sana. Wazee wanahitaji chombo ambacho kitawalinda kwa sababu wametumikia taifa katika ujana wao. Kuna wengine waliokuwa katika jeshi la usalama na jeshi la kulinda taifa la ndani na nje, ambao wameathirika katika shughuli hizo. Kwa mfano, wengi wanapofika umri wa uzee, wanafuatwa na maradhi mengi sana. Wakati askari anapokuwa katika gwaride, anatumia nguvu na kutembea sehemu nyingi, akipanda na kushuka milima. Baadaye, yale maradhi, yanayohitaji kuangaliwa kwa umakini na yaliyo na gharama kubwa ya matibabu, yanaanza kuibuka. Kubuniwa kwa kamati kunaweza kumchunga na kumsaidia ili aweze kuendelea na maisha yake. Wazee wengi, baada ya kustaafu, wanafariki kwa sababu ya hali ngumu. Wengi wao pia wanachinjwa kwa sababu ni wazee na wanasingiziwa kuwa ni wachawi, ilhali ni familia zao zimeshindwa kuwalea na kuwaacha na matatizo. Wakati mwingine, wana ardhi ambazo watoto, ndugu na marafiki wanataka kugawanya. Kamati hii itaweza kuwasaidia wazee kusudi wasiwe na hofu ya kufika uzeeni. Serikali ingebuni sehemu ambayo wazee watakaa kwa pamoja na waweze kuendelea na maisha yao. Wawe na walezi na wapewe majukumu madogo madogo na kazi za hapa na pale ili wasiwe wanangoja tu kufa. Kifo si kwa sababu ya umri. Wadogo pia wanakufa. Lakini, wawekwe katika sehemu ambayo watakuwa na moyo na waweze kukutana na kukumbushana mambo ya zamani na kupata mapato madogo. Bado tunahitaji ushauri wa wazee na kuepuka laana kwa taifa. Mambo mengi yanatufuata kwa sababu tunakosea wazee wetu ambao wanahitaji msaada wetu. Ninaunga mkono kubuniwa kwa kamati ya kitaifa ambayo itawashughulikia wazee. Shilingi elfu mbili ambazo wanapewa haziwatoshi. Wanahitaji usimamizi upande wa matibabu. Mbio unazoweza ukiwa kijana, hupungua ukifika miaka sitini. Kuna watu wengi ambao wametumikia taifa hili na yale maradhi yamewarudia na hakuna mtu anawashughulikia. Ninajua kuwa Kamati hii ikiundwa watakuwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}