GET /api/v0.1/hansard/entries/1347757/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1347757,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1347757/?format=api",
"text_counter": 250,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": "na taratibu nyingi za kuwatetea wazee hao. Katika upande wa matibabu, wakifika umri wa 65 hadi 70, wawe wanatibiwa bure. Hii ni kwa sababu wenye bima, ukiwa na umri wa 60, wanakukataa kwa sababu wanajua umefikia wakati ambao maradhi yanaongezeka. Lakini maradhi hayo yanatokana na jukumu waliofanya kutetea taifa hili. Hao wanajeshi wazee wastaafu walikuwa wakilinda nchi kabla yao. Wako katika jeshi la polisi. Katika makampuni yaliyo katika taifa, wazee walizitetea zikastawi na ndio maana wale vijana wapo pale mpaka leo. Kwa hivyo, ninaomba tuwalinde wazee wetu ili maisha yao ya mbele yawe sawa. Nchi za ulaya zimetenga sehemu. Huwezi kupata mzee anaenda msikitini ama kanisani kuomba. Anatetewa. Huwezi sikia kijana amempiga mzee wake kwa sababu anaona anamhitaji. Mzee anasimamiwa kila kitu maisha yake yote. Nimesimama kuunga Hoja hii kwamba tukitaka baraka na radhi za wazee wetu, waangaliwe vizuri ili taifa letu pia Mungu awe na imani nalo lisonge mbele. Kwa haya machache, ninashukuru Mhe. Spika wa muda. Ahsante."
}