GET /api/v0.1/hansard/entries/1347771/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1347771,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1347771/?format=api",
"text_counter": 264,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Wazee ni watu ambao wamefanya kazi na wamepoteza nguvu zao. Wanafaa kuangaliwa vizuri. Yaweza kuwa watoto wana muda wa kuangalia wazee, na yaweza kuwa watoto wakorofi au wale ambao hawakupata mafunzo vizuri au wakashikana na mambo mengine wasiangalie wazazi wao. Itakuwa jukumu la Serikali kuangalia hao Wazee. Isiwe wamewekwa kwenye vipembe ama wamefungiwa kwenye manyumba. Wazee wakati huo ndio tunaona wengine wanatembea. Ukienda Masaai Mara, na nimefanya kazi Masaai Mara kwa miaka 13, wageni wengi ni wazee. Wakati huo ndipo wamekuja kutembea. Pengine wamekuja na wajukuu wao au wamekuja wenyewe vizere viwili kutembea. Huku kwetu mambo kama hayo huyapati. Unapata vizere hivyo ni vigonjwa, viko nyumbani na vinafanya kazi ngumu."
}