GET /api/v0.1/hansard/entries/1347772/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1347772,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1347772/?format=api",
    "text_counter": 265,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Kama kule kwetu Lamu Mashariki, wazee wetu walifanya kazi ngumu sana. Maanake kazi za kule ni kwenda baharini. Uende baharini ukavute juya. Kuvuta juya ni unavuta kamba mpaka mikono inashika ngudi. Wazee wale wanahitaji matibabu mengi tofauti tofauti. Lakini wazee wetu kusema kweli walifanya kazi nzito na wanafaa kupata matibabu. Hasa wale watu wangu wa Lamu Mashariki hawapati matibabu kwa sababu hospitali ya rufaa ambayo iko karibu kwetu ni Hospitali ya Kenyatta. Utoke mzee wa Kiunga, Ishakani, Mkokoni, Ndahau, Kiwayu na Chandani, hiyo nimesema ni wadi moja. Watoke kule mwisho waje hospitali ya rufaa inaitwa Level 6 na ni hapa Kenyatta. Tunafaa kuangalia zaidi. Mimi ninaunga mkono sana kwa sababu ninajua wale wazee wangu wanaumia zaidi. Kama kuna wengine wanaumia, basi wangu wanaumia zaidi."
}