GET /api/v0.1/hansard/entries/1347777/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1347777,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1347777/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Bwana Spika wa Muda, wakati mmoja nilienda Singapore, na wazee huko hutunzwa vizuri. Madereva wa taxi wote walikuwa ni wazee. Si vyema kumwambia mzee wa miaka 60 ambaye amestaafu kukaa katika nyumba za wazee na kungoja kutunzwa. Kwa nini tusiwape moyo wazee hawa kwa kuwawezesha kufanya mambo mengine mengi baada ya kustaafu? Wazee wakipangiwa mambo ya kufanya katika maisha ya uzeeni, basi watakuwa na maisha bora. Nilitangulia kusema kuwa wazee ni baraka. Binadamu hustaafu, lakini tumbo halistaafu. Tuweze kuweka mikakati ya kuwawezesha wazee kufanya kazi ndogo ndogo. Sisi huambiwa kuwa baada ya miaka 60, watu hukaa na kungoja kifo. Kifo ni hiari ya Mungu; mtu anaweza kufa akiwa kijana au mzee. Tusiwache wazee bila kazi kwa sababu hawatasaidika."
}