GET /api/v0.1/hansard/entries/1347821/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1347821,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1347821/?format=api",
"text_counter": 314,
"type": "speech",
"speaker_name": "Rabai, PAA",
"speaker_title": "Hon. Kenga Mupe",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Ninasimama kuunga mkono Mswada huu wa kubuniwa kwa baraza la kitaifa la wazee. Ninachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Gathoni Wamuchomba kwa kuleta Mswada huu wa maana katika Bunge la Kitaifa. Katika utamaduni wetu wa Kiafrika, tunatakikana tuheshimu wazee kwa sababu ni vioo katika jamii. Kama Mbunge wa Rabai, ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu wazee wetu ambao wamefikisha umri wa miaka sitini katika vijiji wanatengwa na kubaguliwa. Huu ni wakati mwafaka wazee wetu waweze kupata msaada. Ni muhumi Serikali itenge hazina ya pesa ambayo itahakikisha kwamba wale wazee wote ambao wako na miaka sitini wanawezeshwa ili wakimu mahitaji yao ya kimaisha."
}