GET /api/v0.1/hansard/entries/1347822/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1347822,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1347822/?format=api",
    "text_counter": 315,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Rabai, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Kenga Mupe",
    "speaker": null,
    "content": "Wazee hao wapewe bima ya afya ili wahakikishe wanapokuwa wagonjwa, wataenda hospitali na kupata huduma bila kulipa pesa zozote. Hao wazee wanastahili kupatiwa chakula. Wamekuwa ni vioo katika taifa na jamii. Katika eneo bunge langu, wazee wote ambao wamefikisha miaka sitini na zaidi wanaitwa wachawi. Inafikia wakati ambapo wanauawa ili wapokonywe rasilimali zao. Katika Eneo Bunge la Rabai, kuna Wodi ambayo inaitwa Mwawesa. Kuna vijiji kama vile Bwaga Moyo, Ngare na Ngindo ambavyo kufikia leo, kuna wazee zaidi ya mia moja ambao wameuawa kwa sababu wao ni wachawi. Ninaunga mkono Mswada huu. Baraza la kitaifa la wazee litakapoundwa, wazee kama hao watatetea rasilimali zao."
}