GET /api/v0.1/hansard/entries/1347962/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1347962,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1347962/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Mhe. Spika kwa kunipatia hii nafasi ili nichangie hoja hii ya mauaji yaliyofanyika Eneo Bunge la Turbo. Kwanza kabisa, ninatoa risala za rambirambi kwa niaba yangu, na kwa niaba ya wakazi wa County ya Nakuru kwa Mhe. Janet, ambaye ni Mjumbe wa Eneo Bunge hilo. Pia, ninawaambia wananchi wa Kamagut pole kwa shida ambayo iliwapata. Ni ajabu kubwa kusikia kwamba maafisa ambao wanahitajika kudumisha usalama wa wananchi pamoja na mali yao ndio wanatekeleza mauaji kinyama. Hata kama watu walienda kuiba, hawastahili kuuawa. Katika Jamii zetu, baada ya kuvunwa kwa mahindi, watoto na baadhi ya watu wazima huenda mle shambani kuokota mahindi yaliyosalia. Hii ni mambo ya kijamii na ya kibiblia. Kama waliouliwa walienda kufanya hivyo, hayo si makosa. Na hata kama ni wizi, haifai wauawe. Inafaa washikwe, wapelekwe kwenye kituo cha polisi na wafunguliwe mashtaka kortini. Kwa hivyo, nina imani kuwa Serikali yetu itawachukulia hatua na kuwaadhibu, na hata kuwafuta kazi maafisa waliohusika kwenye mauaji hayo. Huwezi kulinganisha maisha na mahindi ama kitu kingine kile. Maisha yanafaa kuchukuliwa na Mwenyezi Mungu peke yake wala sio binadamu. Asante, Mheshimiwa Spika."
}