GET /api/v0.1/hansard/entries/1349604/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1349604,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1349604/?format=api",
    "text_counter": 658,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii nichangie hii Ripoti ya swala la Shakahola. Kwanza, ningependa kutoa pongezi kwa Kamati yote ikiongozwa na Mwenyekiti wao, Seneta wa Kaunti ya Tana River, Sen. Mungatana. Wameonyesha ujasiri na maarifa ya hali ya juu katika hii Ripoti. Hata hivyo, natanguliza masikitiko yangu katika mambo ambayo nimeona yamejiri tangu Shakahola ilipoletwa katitka televisheni zetu. Tumekuwa na matatizo makubwa ya ugaidi na itikadi kali katika taifa letu. Tuliona mambo yaliyotokea wakati wa mlipuko wa bomu na mambo mengine ambayo yameendelea kutokea. Nimeona mfumo tofauti umetumika katika maswala ya Shakahola. Katika Kaunti ya Mombasa, tulikua na tatizo katika Msikiti Musa. Sheikh mmoja alipigwa risasi baada ya kusemekana kwamba kuna mahubiri ya itikadi kali ambayo yalikua yanaendelea katika Msikiti ule. Tuliona polisi wengi wakiingia katika hio nyuma ya maombi. Mambo yalitendeka na hatimaye yule mhubiri, Mwendazake Aboud Rogo, akapigwa risasi. Mpaka leo, hatujui Aboud Rogo aliuawa na Serikali au aliuawa na wale wenzake aliokua akifanya nao biashara ya itikadi kali. Hayo tuyaweke kando. Nimeona tofauti kubwa vile ambavyo Mhubiri Mackenzie amebebwa katika kesi ya Shakahola. Nikizingatia maafa yaliyotokea mbeleni kisha nilinganishe na yaliyosemekana yalifanywa na wahubiri ya dini ya Kiislamu, ni tofauti na vile kesi ya Mhubiri Mackenzie imetekelezwa. Mpaka sasa, Mackenzie yupo na hatujaona mashtaka ambayo amefunguliwa. Hatujui kama atafunguliwa mashtaka. Kulikuwa na mjadala wazi katika televisheni ya kwamba hakuna kesi ambayo anaweza kufunguliwa kwa sababu watu ambao aliwaangamiza kupitia mahubiri yake, walienda huko kwa hiari. Langu tu ni kutoa mtazamo na fikra yangu, ya kwamba ni tofauti sana jinsi kesi ya Shakahola inavyotekelezwa ukilinganisha na kesi zingine ambazo tumekuwa tukiambiwa ni za ugaidi na itikadi kali. Nikizingatia idadi ya watu ambao wameathirika, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}