GET /api/v0.1/hansard/entries/1349605/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1349605,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1349605/?format=api",
"text_counter": 659,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Shakahola tumepoteza Wakenya zaidi ya 800. Hebu ongeza idadi ya maafa yale mengine ya ugaidi hapo nyuma, ambayo yamekuwa yakiangaziwa kwa mda. Bi Spika wa Muda, ugaidi ama itikadi kali sio wa dini ya Kiislamu pekee. Dini yoyote na mhubiri yeyote anaweza kuamua kufundisha watu mambo ambayo hayapo katika vitabu vyetu vitakatifu. Ningependa kuipongeza pia Kamati kwa Ripoti hii kwa sababu wamekuja na mambo ambayo yananipa moyo kama mzazi katika hili taifa. Wamesema, ipo haja ya sisi kama wazazi kufuatilia ni mafunzo gani ambayo watoto wetu wanafundishwa na hawa wahubiri tunapowapeleka kufunzwa mafunzo ya kidini. Hata mimi nimeleta Mswada hapa wa Child Parent, yaani mtoto ambaye amepata mtoto akiwa bado ni mtoto, aweze kurudi shule kwa sababu haya yote, kwa mtazamo na fikra yangu, tunayapitia kwa sababu watoto wetu na sisi wenyewe hatuna elimu ya kutosha ya kujisomea vitabu vitakatifu. Watu walioangamia pale wangekua wamepata elimu ya kutosha, hata tu ya msingi, hawangepotoshwa hadi kufikia kuangamia. Hali zetu za umaskini pia zimechangia pakubwa katika Wakenya wamepoteza maisha yao vile walivyopoteza. Walipewa fikira ya kwamba, watakapokuwa pale, watakutana na Yesu mapema. Hio inaleta uvivu ya kwamba, heri niende na Yesu na mimi niende peponi. Ingekua ni mtu anapata mlo mara tatu kwa siku na elimu ya kutosha ya kuweza kujisomea kitabu kitakatifu, hawa Wakenya wenzangu hawangeangamia kule. Bi. Spika wa Muda, ningependa kusema ya kwamba wale tunaowapa mamlaka ya kufundisha ama kuwa wahubiri katika madhebahu yetu, wawe ni watu waliyopitia mfumo fulani na kupewa kibali cha kupeana mahubiri hayo. Japo tuko na uhuru wa kujihusisha na dini tunayoipenda na tunayoitaka, tumeona madhara makubwa sana ya kuachilia hii idara ya dini yetu kuwa huru. Tumeona hata watu wengine wamefungua biashara ya kuwauzia watu kitu kama maji kwa pesa, na wamejitajirisha wao wenyewe na kuletea Wakenya wengine madhara. Hivyo basi, naipongeza kamati hii nikisema ya kwamba, sheria ni msumeno. Lile linalo fanyiwa dini moja, basi lifanyiwe dini zote. Kosa ni kosa na hakuna kuhesabiwa haki kwa kosa. Ikiwa kuna mtu ameangamiza Wakenya, hatua ichukuliwe kama ilivyochukuliwa kwa wale wengine waliyotangulia dhidi ya makosa yayo hayo. Asante."
}