GET /api/v0.1/hansard/entries/1349961/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1349961,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1349961/?format=api",
"text_counter": 305,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Tusiwasumbue hawa ndugu zetu kwa maana roho zao ni ndogo na zinapata mtihani wanapoona vitu kama vile. Kwa hivyo, mavazi hapa Bungeni ni kama ulivyosema. Wanawake nguo zipite magoti. Mkatae mkubali, hiyo ndiyo heshima ya Wabunge walioko Bungeni. Kuhusu kauli mbiu ya My dress, My choice, ukiwa kwako nyumbani, hata chumbani mwako waweza kukaa hivyo hivyo ama ukavaa unavyotaka ukiwa na mume wako. Tukiwa ndani ya Bunge, tunastahili kufahamu kwamba sheria zimetungwa ili tuweze kuzifuata. Ni sheria zilizowekwa kutunza heshima ya Bunge la Taifa ili liwe katika anga za juu. Mimi kama Mama Kaunti wa Mombasa, nimefurahi maanake mimi mwenyewe naelewa kwamba nikijifunika, sitoi mtihani kwa watu. Pengine dada zangu waliopotea njia na kuvaa spaghetti na nguo za mikono mifupi hawakuwa wanajua. Leo wamepata mwelekeo. Kwa hivyo, tuvae kwa heshima na tuheshimu Bunge la Taifa."
}