GET /api/v0.1/hansard/entries/1352672/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1352672,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1352672/?format=api",
    "text_counter": 2432,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Malindi, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii nizungumze kuhusu hii Ripoti ya Kamati ya Deni la Umma na Ubinafsishaji. Kama kiongozi mchanga, kwa sababu ni mara yangu ya kwanza kuchaguliwa katika Bunge la Taifa, nina wasiwasi mkubwa sana kuhusu madeni ambayo tunajiwekea kama taifa. Takriban miaka 20 ijayo, maisha ya Wakenya yatakuwa magumu zaidi. Hii ni kulingana na zile pesa ambazo Serikali yetu ya Kenya inaomba kila mara. Waswahili husema dawa ya deni ni kulipa. Kwa hivyo, haya madeni yote tunachukua, dawa yake ni kwamba lazima Wakenya wayalipe. Tusipolipa sisi, inamaanisha ni watoto, wajukuu au vitukuu wetu ambao wataumia kwa kulipa madeni ambayo tunachukua sasa. Nimeangalia Ripoti hii vizuri. Inaonyesha kuwa kati ya mwezi wa Mei 2022 na Aprili 2023, Ksh213.24 bilioni zilikopwa. Ni lazima pia sisi tueleze kuwa serikali ya handshake kwa kipindi cha mwaka mmoja ilichukua Ksh1.6 bilioni. Inamaanisha kwamba pesa ambazo tunakopa kwa sasa zimeongezeka zaidi. Ukilinganisha Serikali ya Kenya Kwanza na ile serikali ya handshake, kuna tofauti kubwa ya pesa ambazo zimekopwa. Kabla ya kukopa pesa kule nje, ni lazima tuangalie pato letu la kitaifa liko vipi. Pato letu la kitaifa ni pesa ambazo zinaweza kustahamili mikakati yote inayohusu jinsi ambavyo mikopo italipwa. Serikali inajua kuwa kuna namna nyingi ya kupata pesa. Jambo la kwanza ni Serikali iweze kuongeza ushuru. Lakini jambo hilo la kuongeza ushuru tumelikataa kama watu wa Azimio. Hatutaki kuongezewa ushuru kwa sababu tayari bei ya maisha iko juu. Mbinu ya pili ambayo Serikali inaweza kupata pesa ni kupunguza matumizi. Jambo la tatu la kusaidia The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}