GET /api/v0.1/hansard/entries/1352677/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1352677,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1352677/?format=api",
    "text_counter": 2437,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Malindi, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
    "speaker": null,
    "content": "kilikuwa ni Ksh10 trilioni. Sasa hivi kiwango hiki kimeondolewa. Katika hiyo Ksh10 trilioni tuko na deni ya Ksh9.6 trillion . Iwapo kiwango hiki cha juu kabisa hakingekuwa kimeondolewa basi Wakenya tungekuwa tumetahayari kwa sababu hatungejua ni vipi tungelipa madeni haya. Kutolewa kwa kiwango hiki ni hatari sana kwa sababu sasa hivi ni mambo mengi sana ambayo hayaeleweki. Tunapokopa pesa hizi, ni vyema tujue jinsi tutazilipa. Jambo hili linapaswa kuwekwa wazi ili Wakenya waelewe nia ya mikopo na mikakati ipi imewekwa kuhakikisha mikopo hii imelipwa. Ripoti hii haijaangazia mikakati kama hiyo. Tunakopa tu bila kufikiria jinsi mikopo hii italipwa. Mikopo hii pia haina uwazi. Wakati wa kwenda kuchukua mikopo, ni watu wachache tu huhusishwa lakini sote, wazee kwa watoto, wanawake kwa wanaume tunatarajiwa kuilipa. Sifurahii jambo hili. Tunataka uwazi. Waziri wa Fedha anapoulizwa kuhusu deni la umma, yeye hupeana tu hadithi. Hatujawahi kuona agreements kati yetu Wakenya na nchi zinazotufadhili. Takwimu kama hizi ni lazima ziwe wazi ndiyo Serikali inapoeleza kuna madeni, tunajua ni yapi na ni pesa ngapi tunapaswa kulipa kila mwezi au kila mwaka. Serikali yetu ni lazima iwache kutegemea misaada kutoka nje. Misaada hii ndiyo inatusukuma kama nchi leo. Hivi leo, tukitaka pesa kutoka nchi fulani, ni lazima tupitishe sheria za ushoga na usagaji, kwa kimombo LGBTQ. Tumekataa kujitegemea na basi tunawekewa sheria ngumu ngumu kama hizo. Kwa kukubaliana na sheria ambazo hata sisi hatuzielewi, tunaipoteza nchi yetu. Hapo zamani, utalii ulikuwa unaleta pesa nyingi sana hapa Kenya. Sasa hivi, watalii wamekimbilia Tanzania na Zanzibar na sijasikia mikakati yoyote kwenye Ripoti hii ya kufufua utalii wetu. Leo hii hatuna pesa za kigeni za kutosha. Tungeweka mikakati katika sekta ya utalii, angalau tungekuwa na afueni kama Wakenya. Kila siku tunadanganywa kuwa pesa zinakopwa ili kufanya miradi. Ukweli ni kuwa matumizi ya mikopo hii ni mabaya. Ufisadi ni mwingi sana nchini. Mikopo hii ni deni lakini haitumiwi kufanya miradi ya kusaidia watu bali pesa hizi zinaishia katika mifuko ya watu. Jambo hili la ufisadi pia linanisikitisha sana. Pendekezo langu ni mikopo hii ipitishwe na Bunge la Kitaifa. Sisi huketi hapa na kugawa na kuidhinisha matumizi ya pesa nchini. Vile vile tunahaki ya kujua mikopo hii inachukuliwa vipi ili tuipitishe. Sisi ndiyo sauti ya wanyonge. Sasa hivi, anatupatia hadithi pasipo na mwelekeo mzuri. Ombi langu lingine ni tuweze kufanyia deni la umaa ukaguzi, yaani audit. Tufanye ukaguzi wa deni la umma ili tuelewe ni wapi tulipo na ni vipi tunaweza kujiondoa kwenye hii shida. Asante sana Bwana Spika wa Muda."
}