GET /api/v0.1/hansard/entries/1352696/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1352696,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1352696/?format=api",
    "text_counter": 2456,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kapenguria, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Samwel Chumel",
    "speaker": null,
    "content": "Ukiangalia wale wanaenda kuomba, ni kweli vile watu wanasema. Kwamba, pesa nyingi zinaingia lakini hatuoni zinafanya nini. Ninatoka sehemu ya North Rift. Kule ni Aridand Semi-Arid Lands (ASALs). Vita unavyosikia watu wanapigana na kugombana ni kwa sababu ya shida na umaskini ulioko katika sehemu ile. Watu wanaumia. Badala mtu afe njaa, anaona ni afadhali aende kwa jirani akachukue mboga ya watoto. Hiyo imeleta shida. Tunajua shida itapungua chakula kikiwepo. Ninakumbuka kuna wakati tulipitisha hapa kwamba askari jeshi na polisi waende kusaidia kuweka usalama katika eneo hilo. Ukienda huko saa hii, utapata watu wakilia kuwa hawana mafuta au hiki na kile ilihali kuna pesa tulipeana. Hatujui ilienda wapi. Kazi yetu hapa ni kutazama, kutoa macho, na kuangalia ni nini kinafanyika. Pesa lazima imfae mwananchi. Hii pesa si ya mtu. Ni raia walitoa kodi na jasho lao. Lazima tuone kwamba ile jasho wanapata ni ya ukweli—wapate haki yao na wafurahie. Ndiyo maana ninasema tusiwe nyumba inayoongea tu, a talking House. Tusiwe nyumba inayoongea na kutengeneza Ripoti kama hii ambayo inakusanya vumbi tu. Lazima tufuatilie na wakati mwingine tuulize hizo Kamati kuhusu zilipofikisha baadhi ya mapendekezo ya Ripoti zao. Isije ikawa tunaongea tu na watu wanatazama. Saa nyingine wananchi wanapata mawazo safi tukiongea. Wao huanza kuwa na matumaini kwamba inaonekana kuna mwelekeo mzuri. Mwishowe hakuna mwelekeo. Ninahimiza Nyumba ya sasa, the current Parliament, iwe na watu wawezao kusema ukweli bila kuficha lolote. Kuna wakati hungesema kitu hapa kwa sababu nyumba ilikuwa upinzani kule na serikali hapa. Lakini saa hii utapata kwamba hata kiongozi anayetoka upande wa Walio Wachache anabebwa na gari la Serikali. Kwa hivyo, sisi sote ni Serikali. Tuweke nguvu yetu pamoja. Niliona yule kijana wangu ambaye tulimweka kuwa Kiongozi wa walio Wachache katika Bunge hivi majuzi, leo anatembea na gari la Serikali. Nilimwambia, “Basi, Serikali hukaa namna hiyo”. Kitambo usingeona mtu wa Upinzani na mtu wa Serikali pamoja. Hawangeweza kuangaliana ilihali sisi sote ni Wakenya. Sasa sisi ni nyumba moja. Ukiangalia yaliyoandikwa hapa, hii Nyumba ni ya Wakenya ambao ninataka wafurahie. Sitaki kusema zaidi. Ninataka niunge mkono na kushukuru hii Kamati. Twende namna hii na kuweka nguvu zaidi mpaka tufaulu. Juzi tumesikia kuna mama anahangaishwa kwa sababu ya mafuta ya Ksh17 billion. Ninashukuru wale walifukuza watu wa kanisa. Watu wanaenda huko kusema haleluya na hali walifanya dhambi jana. Mimi ninaweza kurarua watu kama hawa. Asante."
}