GET /api/v0.1/hansard/entries/1352699/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1352699,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1352699/?format=api",
"text_counter": 2459,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "kila siku. Kila uchao ni madeni. Madeni yakichukuliwa na taifa, kawaida huwa yanakusudia uzalishaji zaidi. Hivyo, madeni hayo huweza kulipwa. Deni huchukuliwa kwa sababu ya mambo ya maendeleo, kujenga taifa na kutoa mzigo ambao Mkenya angetozwa kama ushuru zaidi. Inasikitisha kuwa pesa zinabadhiriwa licha ya kuwa madeni yamekuwa makubwa. Kutoka Septemba 2022 mpaka Aprili 2023, inasikitisha kuwa deni la ndani ya Kenya limefika Ksh4.7 trilioni. Nikilinganisha na serikali iliyoondoka, hiyo ilichukua deni ya Ksh6 trilioni kwa miaka kumi . Kwa mwaka mmoja tu, tayari Serikali hii imetutia deni la Ksh4.7 trilioni la ndani. Inasikitisha kasi ambayo Serikali hii inachukua deni ukilinganisha na mazao tuonayo. Ninazungumzia takwimu ninazoangalia hapa. Hakuna makosa kwa Serikali kuchukua deni. Serikali inaweza kuchukua deni ikiwa inakusudia mema."
}