GET /api/v0.1/hansard/entries/1352703/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1352703,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1352703/?format=api",
"text_counter": 2463,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante Mwenyekiti wa Kamati iliyoandaa Ripoti hii. Ndiyo maana nikasema hili ni deni la ndani. Sikusema deni la nje. Nimesema deni la ndani. Bado hii yote inasikitisha kwa sababu Wakenya wamekamuliwa sana. Nikifikiria kama Mama wa Kaunti ya Mombasa, wajukuu wangu ama vitukuu vyangu watakuja kudaiwa pesa ambazo hawazijui. Inaonyesha Serikali ama taifa haliendi vizuri ikiwa deni lachukuliwa hapa kulipa kule. Linalosikitisha hata zaidi ni kwamba sisi Wabunge tunajadili Ripoti kuhusu madeni ya Kenya ilihali Bunge halihusishwi wakati wa kuchukua madeni. Kama Mheshimiwa katika Bunge, naomba tuhusishwe kupiga msasa na kuuliza maswali kuhusu madeni yoyote ambayo Serikali inatarajia kuchukua ili tupinge kama si deni la dharura. Twafaa tuulize maswali na tujue kwa nini deni au mkopo unachukuliwa. Je, ni deni la dharura? Ikiwa litakuwa deni la dharura, tutaelewa ikiwa Serikali haina namna. Nimeona World Bank ilileta msaada wa Ksh16 bilioni. Nimeona wakizungumzia visima katika sehemu ambazo zimeathiriwa na ukame lakini watu wa sehemu hizo wanalia kuwa hawajapata hivi visima. Ni utata mkubwa kwa sababu kila mwaka tunasema Ksh700 bilioni zinapotea. Hivi ndivyo pesa hupotea. Mhe. Spika wa Muda, Serikali inaweza kuwa na nia nzuri ya kuchukua pesa. Lakini hizi pesa zinapotelea katika mifuko ya watu na hazileti natija kwa taifa. Ninasikitika kama mama katika taifa hili kuona kuwa pesa zinabadhiriwa kiholela. Pesa zinachukuliwa na kwenda kwa mifuko ya watu. Kumbuka hali ilivyokuwa ndani ya Jomo Kenyatta International Airport juzi. Maji yalikuwa yanamiminika na kumwagika. Ilikuwa aibu kwa taifa hili kuona wageni wanaingia huku wananyeshewa ndani ya airport, wala siyo nje wakitoka kwenye ndege. Walinyeshewa wakiwa ndani, kwenye check-in. Wageni wanamwagikiwa na maji wakati tunajua pesa za ukarabati na kufanya mambo haya zipo. Lakini hatukuona natija yake yoyote pale airport. Ilikuwa aibu. Kuna aibu nyingine. Sisi tumeona mvua kubwa sana Kaunti ya Mombasa. Kama Mama Mombasa Kaunti, ninatuma rambirambi zangu na pole kwa wale waliofiwa na jamaa zao. Pole kwa waliopoteza mali yao. Awali ya yote ni kwamba ninasikitika kuwa hapa hapa kuna Mbunge, Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Uidhinishaji wa Matumizi, ambaye amesema kuwa Ksh6 bilioni zilikuwa za disaster management. Hizi pesa hazikufikia magavana."
}