GET /api/v0.1/hansard/entries/1352705/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1352705,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1352705/?format=api",
"text_counter": 2465,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "kwa pesa na aseme amezileta. Alianza kwa kuwasingizia magavana na kuwashurutisha watumie pesa zilizotengewa maendeleo katika kaunti kushughulikia janga la mafuriko. Kila senti zinapotolewa katika kaunti huwa zinashughuli zake. Gavana akitumia pesa za mishahara leo kushughulikia janga la mafuriko ataleta shida nyingine kubwa. Wafanyikazi wa kaunti wakikosa mshahara leo, itakuwa tena izara katika taifa nzima. Hili lilinifanya nikatamaushwa sana, kama Mama wa Kaunti ya Mombasa. Sikupenda zile tetesi zilizokuwa zikiendelea kwa sababu ya pesa ambazo zilikuwa katika Bajeti. Pesa zozote zinazokuja katika taifa hili kwa msaada wowote zina malengo yake. Pesa hizo zinafaa kutumika kutimiza malengo ambayo yamekusudiwa."
}