GET /api/v0.1/hansard/entries/1352706/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1352706,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1352706/?format=api",
    "text_counter": 2466,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "Pesa zinazoibiwa ni nyingi. Tumezungumza hapa leo na ikatamausha sana kumsikia Kiongozi wa Wengi Bungeni akiita mwandishi wa habari illiterate. Matamshi kama hayo hayafai ndani ya Bunge hili. Wale waandishi wa habari wanaoonekana kuwa illiterate ndio wanaolipa ushuru na wanafinyika kule chini. Tuheshimu Wakenya wote. Maskini ama tajiri apewe heshima yake. Nimeangalia tena katika Ripoti hii nikaona kuwa pesa zilitengwa za kujifunza ujuzi ambao unagusia Jumuia ya Afrika Mashariki. Lakini sijaona mambo haya yakitendeka ndani ya Kaunti ya Mombasa. Haya ndio yale tunasema Makadirio ya Bajeti yanakuja lakini hayaendi kwa wale wamelengwa. Kila Mkenya ni mtoaushuru. Kila anayetoa ushuru ni lazima matumizi ya pesa yamfikie kule chini. Ninajua kwamba kati ya malengo ya kukopa pesa ni kuweza kuzuia Wakenya kulipa ushuru wa juu. Lakini kutoka hivi karibuni, ushuru mkubwa sana unatozwa Wakenya hadi wanalia sasa. Ushuru umeongezeka. Kila kitu kimeongezeka bei. Deni pia limeongezeka. Kitu ambacho ninaweza kupongeza katika Ripoti hii ni zile pesa zilizoenda kwa wakulima kwa sababu walikuwa wanazihitaji sana ili tuweze kuleta mazao na taifa lipate chakula. Pia, ninatoa pongezi kwa zile pesa ambazo zimeenda kwa sekta ya afya. Watu wanahitaji afya bora. Kuna vifaa ambavyo vinatumika ndani ya hospitali. Kuna hospitali nyingi ambazo hazijapata vifaa hivyo. Pengine wananchi ni watano na mwizi achukue kumi. Hayo ndiyo mambo ambayo yanaendelea katika taifa hili. Kwa hivyo, mimi ninapinga, haswa uchumi mbaya na Serikali kukopa kila siku na kwa kasi sana. Iwache kuombaomba. Pesa ambazo wanatoa kwa mwananchi, wawekeze mahali ambapo ni sawa na wananchi waweze kupunguza ule uzito wako nao. Deni likiendelea hivi, litakuja kutusumbua. Mkisikia wananchi wanalia kule chini, tuwaelewe. Tusiwapelekee mambo ya ubishi. Hao ndio walituchagua. Leo tuko Bungeni na wananchi wanalia hali ni mbaya. Tusigombane hadharani kuonyesha mambo ambayo sio sawa wakati wananchi wanahangaika. Ninamalizia kwa kusema kwamba dawa ya deni ni kulipa. Kama tumeamua kulipa deni, basi tusiwafinye wananchi. Pesa tulizozichukua kama mkopo, ni lazima tuletewe hapa na waje hapa Bungeni watuambie zilienda sehemu fulani, mazao yake ni haya, tumebaki na pesa kiasi fulani na tunadaiwa pesa kiasi fulani. Lakini, mambo ya kuletewa tarakimu ambazo zimeandikwa na sisi hatujui pesa zimetumika vipi, hatuwezi kubali katika Bunge la Kenya. Wakenya wanatuangalia sisi. Walituamini na wakatupigia kura. Tuliweka ahadi kuwa tutakuja kuwapigania. Leo hii, angalia Bunge lilivyo wazi. Tukileta Hoja katika Bunge hili ya kumfinya mwananchi, Bunge huwa limejaa Wabunge wa kusema ‘aye.’ Hoja inahusu mwananchi leo na wote wameenda kufanya biashara zao. Mimi ninachukia hali hii. Ninawaambia Wabunge wenzangu, haswa Wabunge wa Kenya Kwanza, kuwa hii sehemu yao iko tupu. Inaonyesha vile nyinyi hamuwafikirii Wakenya na wale wanaohangaika kule chini. Ninasikia kulia. Hoja hii inahusu mwananchi wa chini. Ninawaambia chuma ni chenu. Mtarudi kule kwa wananchi kutafuta kura na mtapata majibu yenu."
}