GET /api/v0.1/hansard/entries/1353075/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1353075,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1353075/?format=api",
"text_counter": 291,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "walimwuliza, “umebeba nini” akasema “Nimebeba vitu vya kawaida.” Wakamwuliza lakini hiyo ni nini.” Akasema kuwa ni unga tu; kwani kuna shida gani? Wakamwambia, “Hatukubali unga.” Akawaambia lakini huu ni unga wa Jogoo” wakasema unga wa Jogoo haukubaliki hapa. Na hakuweza kuingia nayo. Standards zao kule ni tofauti kidogo na standards za kule Malawi. Bi. Spika wa Muda, nitatoa mfano mwingine tena. Kakangu ni mtu wa kusoma sana. Ni profesa wa Economics na anafanya kazi Afrika Kusini. Miaka ile alipokuwa mdogo na alipokuwa antafuta usomi, alienda Germany kufanya shahada yake ya tatu. Alikuwa hajui Kijerumani. Kwa hivyo aliingia dukani, akanunua chakula, nyama na vinginevyo akaenda kupika kama kawaida ya watu wote pale. Basi akatuandikia barua. Miaka hiyo ilikuwa hakukuwa na SMS, W hatsApp ama simu za rununu. Miaka ile tuliyoishi sisi unajua; ulikuwa unaandika barua na kisha unangojea majibu. Akaandika barua na akatuambia kuwa, “Aa! Maisha huku mazuri sana, nyama ni bei rahisi sana.” Tukamwambia kuwa ni vizuri na ikakaa kama mwezi mzima hivi. Baadaye, akaandika barua ya pili, akasema, “Ee! Familia, ile nyama niliyokuwa ninanunua kwa kama wiki mbili, nilikuwa sijasoma vizuri, lakini ilikuwa ni pande ya wanyama wa nyumbani (pets), nami nilikuwa ninanunua ile nyama kwa sababu ilikuwa ya bei rahisi. Hata hivyo, ndugu yangu hakuwa mgonjwa. Alipojua Kijerumani vizuri, alianza kununua nyama mahali pa sawasawa. Hakuwa mgonjwa kwa sababu ya zile standards ambazo wanaweka upande ule wa nchi zilizoendelea. Hapa Kenya, mimi ni mmoja wa wale watu ambao wanapenda kula njugu na sipendi zile njugu za supermarket; ninapenda njugu hizi ambazo tunazipata barabarani. Mhe. (Dkt.) Khalwale anajua wakati wa campaign, ukiwa barabarani, unakula ile ambayo inapatikana. Ukienda na uone kitu chochote, unakula. Tunashukuru Mungu kwa sababu mpaka saa hii, sijawahi kupata ugonjwa baada ya kutafuna njugu, ama chaluka cha barabarani. Wakati umefika sasa kwa sisi Wakenya nasi tuingie katika jumuia ya nchi ambazo zimeendeleaa, ambazo zinatoa standards za chakula ambacho sisi tunakula ili yule ambaye anauza njugu barabarani, yule ambaye anaoka mikate pale barabarani; yule anapika chakula pale nje, tukila chakula chake awe ni mtu ambaye amepimwa na chakula chake kimekubalika. Hii sheria inasema kwamba kutakuwa msimamizi ambaye atasimamia mambo haya ya usafi na standards za chakula. Kwa hivyo, ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu utasaidia Wakenya wengi sana. Wakati tulipokuwa na COVID-19, wengi wetu tuliingia katika mazoea ya kuosha mikono yetu. Kila tulipokuwa tunaosha mikono ama ukipita mahali ambapo kuna hizi dawa za kudisinfect mikono, unaosha mikono yako. Bi. Spika wa Muda, ukweli ni kwamba mambo ya kukohoa na mafua wakati huo yalipungua kwa sababu ya usafi ambao watu walifanya ni mazoea. Tukiingiza standard"
}