GET /api/v0.1/hansard/entries/1353078/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1353078,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1353078/?format=api",
    "text_counter": 294,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "a usafi katika vyakula ambavyo vinapikwa kila mahali, watu watazoea. Standards zetu zitakuwa juu. Hata tukiwa tunapika nini na watu wako barabarani ama kwa hoteli, watakuwa na ile imani ya kwamba katika hii nchi ya Kenya, mambo ya vyakula vyao vinasimamiwa sawasawa na sheria. Kuna vipengele ambavyo viko katika sheria hii ambayo ingekuwa vizuri waviangalie zaidi. Hii ni kwa sababu vinaweza kuleta mushki kati ya serikali gatuzi na ofisi hii ambayo tunaunda kupitia kwa hii sheria. Kwa sasa, vyakula vyote ukitaka kufanya biashara ya hoteli au kufungua kibanda, wanataka uende kwa countygovernment. Mpaka sasa, ukweli ni kwamba watu wetu lazima wapate leseni kutoka kwa serikali gatuzi. Kama hapa Kaunti ya Nairobi, ukitaka kufungua hoteli, lazima uende pale na wanakupatia conditions. Wanakuambia watu wako wakiwa wanapika au kupakua chakula lazima wavae zile kofia, wasiweke makucha marefu na mambo kama hayo. Ikiwa tunaweka ukaguzi wa vyakula katika sheria hii, ni lazima tuangalie hiki kipengele cha 16 ambacho kimezungumzia kuhusu kazi za serikali g Tunataka iwe sawa na vile mambo yako saa hii. Kwa ufupi, tusiweke sheria ambayo itagongana na mipangilio ambayo tayari iko. Serikali gatuzi kama iko na mipangilio yake, ingekuwa vyema hasa wakati wa public participation ya hii sheria, waite serikali gatuzi na Councilof Governors watoe maoni yao kwa urefu kuhusu hiki kipengele cha 16. Sisi Maseneta ambao kazi yetu haswa kaika Katiba ni kusimamia na kusaidia serikali gatuzi, hatutaki tutengeze sheria ambayo iwe tena inaiumiza. Hii sheria inasema ni lazima watengeze ripoti za safety za kaunti; food and feed safety. Hawasemi ni kwa muda gani; mwaka ama mwezi? Wanasema ni lazima wazitengeze. Hawaelezei ni"
}