GET /api/v0.1/hansard/entries/1353080/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1353080,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1353080/?format=api",
    "text_counter": 296,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "gani ambazo hizi ripoti za usafi wa vyakula wa sehemu gatuzi wala ni nini haswa hii sheria inataka. Ukiandika tu laini moja ambayo haijielezi, unaleta shida kwa serikali gatuzi. Hiki Kipengele cha 16 ni lazima wajieleze vizuri. Wakisema watasimamia, wafanye evaluation of a multiannual na hawaelezei hii plan wanataka iandikwe nini au kama kuna regulations ambazo zitawekwa na hawaelezei kwa undani zaidi vile mambo yatafanywa na serikali za kaunti, hiki Kipengele cha 16 kitaleta mushkin katikati ya serikali gatuzi na Serikali Kuu ya Kenya haswa kwa ofisi ya msimamizi wa usafi wa vyakula hapa Kenya. Ningependa sana wakati ambapo hii sheria inaenda kuangaliwa kwa undani, wakati wa public participation, hii sheria iwekwe chini na watu wa kutoka sehemu gatuzi wapewe nafasi waongee zaidi na watoe mawazo yao. Pia, ninaomba ile kamati ambayo itashughulikia hii sheria kutoka kwa Seneti, Seneti tumekuwa na mazoea ya kwamba wakati wanaita watu kufanya publicparticipation, wanaenda kwa vikundi ambavyo vimejulikana; county government,Council of Governors, Law Society of Kenya na makanisa. Hao ndio wanawaita stakeholders. Ninaomba wakati hii Kamati inakaa, waite hawa watu wadogo ambao wanafanya hizi kazi wawasikize ili wasiweke masharti ambayo yatagandamiza wafanyikazi na wafanyibiashara; yule mama anayepika pale vibandani, wale vijana ambao wanapata"
}