GET /api/v0.1/hansard/entries/1353082/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1353082,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1353082/?format=api",
"text_counter": 298,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "vyakula vyao kwa kuuza korosho, njugu au mahindi ya kuchoma barabarani tungependa maoni yao pia yazingatiwe. Sio wakubwa peke yao ama Kamati iandae mikutano katika hoteli kwa organizations kubwakubwa. Chukueni watu wa kawaida muwasikize maoni yao ili tusije tukapitisha sheria ambayo itamgandamiza mwananchi wa kawaida. Naomba sana wakati wa public participation, hili jambo lifanyike. Waite watu wa kawaida ambao sisi tunawajua. Watu kutoka nyumbani wengi wana hustle hapa Kaunti ya Nairobi na tunawajua. Tukiambiwa tuwalete, tutawaleta ili nao watoe maoni yao. Jambo lingine kuhusu hii sheria ni haizungumzii chakula cha binadamu pekee; inazungumzia chakula cha wanyama ambao sisi tunawala kama kuku, mbuzi na kadhalika. Hivi vyakula vya wanyama haviwekwi katika standard yoyote. Sisi tunaambiwa ukienda supermarket, utasema hii ni chakula ya paka au mbwa na unanunua. Lakini hakuna competent authority ambayo inafanya sisi tuwe na imani ya kwamba vyakula hivi ambavyo tunapatia wanyama wetu, haswa wale wanyama ambao wanatuletea pesa kama kuku, mbuzi na ng’ombe, viko katika standards ambazo zinatakikana. Kitu kimoja tu ambacho ningependa kuongezea kwa hii sheria ni kuwaomba wale wameileta hii sheria watengeneze mahali ambapo kutakuwa kukifanyika research . Hakuna kipengele chochote ambacho kinahusika na utafiti. Hakuna mahali ambapo hii ofisi ambayo tunaitengeza ya usafi wa vyakula imezungumzia kuhusu utafiti. Tunataka tuwe na kipengele ambacho kitaongea kuhusu utafiti na utafiti huu usaidie katika kutengeneza standards ambazo zitawasaidia Wakenya. Ikiwa tunakula chakula barabarani, kwa mikahawa au hotelini, ziwe zinafika pahali pazuri. Pia, kuwe na standard ambayo tunajua kama mtu anakula hapa, kibali chake kinaonyesha kwamba huyu mtu chakula chake kimepitishwa na usiwe na wasiwasi unapokula. Tukiona hii sheria imepita, tutafurahi kwa sababu itakuwa inaleta Kenya kwa kiwango cha nchi ambazo zimeendelea kwa usafi wa vyakula ambavyo vinaleta afya nchini na kwa wananchi wao. Kwa hayo mengi, naomba kuunga mkono sheria hii ambayo tunayounda. Naomba wenzangu wanaonisikiza pia waiunge mkono na wakati wa kuupitisha sheria hili. Asante, Bi Spika wa Muda."
}