GET /api/v0.1/hansard/entries/1353571/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1353571,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1353571/?format=api",
    "text_counter": 437,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": ". (Kisauni, ODM): Asante sana, Mheshimiwa Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili niweze kulizungumzia swala hili. Nimesimama kuunga mkono kuongezwa kwa viumbe wa baharini katika orodha ya wanyama ili watu walipwe fidia wakati viumbe hao wamewadhuru, au kuleta madhara, majeruhi au vifo. Hapakuwa na usawa hapo mwanzoni kwa sababu karibu wanyama pori wote wa ardhini, walikuwa wameorodheshwa ili watakapoleta majeruhi, madhara au kifo, watu walipwe fidia. Mnyama mmoja wa ardhini ambaye ametolewa kwa orodha hiyo, na ambaye nitaomba oangezwe, ni nyoka. Nyoka pia anadhuru wananchi. Hakuna kiumbe mmoja wa baharini ambaye alikuwa amewekwa katika orodha hiyo ili akimdhuru binadamu au kumtoa maisha, binadamu alipwe fidia. Kuna sehemu ambazo misitu yao ni bahari iliyo karibu na wao. Ukiangalia papa, huwa ni wanyama ambao wanakuja kwa bahari ya maji madogo. Wanafuata meli kubwa zinapokuja wakitafuta chakula. Meli ikifika wanatembea katika maji madogo na watu wengi wamekatwa miguu na kupoteza maisha yao, ila hawalipwi fidia. Wanaambiwa viumbe vya baharini havilipiwi fidia, ilhali wale viumbe wanalindwa na sheria. Kwa sababu ukimchukua papa ukamlee nyumbani utafungwa. Kama huyo ni mnyama pori, kwa nini akifanya madhara mtu asilipwe? Kwa hivyo, ni vyema kuwaongeza wanyama kama papa, samaki wa mawe, nyangumi na samaki ambaye akikudunga mwiba wake, mpaka ukatafute sindano ya tetanus ama mguu utaoza."
}