GET /api/v0.1/hansard/entries/1353572/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1353572,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1353572/?format=api",
    "text_counter": 438,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Nasimama hapa kuhakikisha kuna usawa katika sehemu kama Lamu, Mombasa, Shimoni na nyingi ambazo maji ndiyo yamechukua nafasi kubwa. Lazima watu walipwe fidia wakati wanyama hawa wataleta madhara. Ikiwa halipwi basi tupe ruhusa tufuge papa kwa nyumba zetu. Tutengeneze maji na tumlete akae pale. Na ikiwa ni makosa kisheria, basi tulipeni wakati mtu amepatikana na hiyo shida. Juzi kuna mtu ambaye amekatwa mguu katika sehemu ya ferry kivukoni, saa zingine papa huleta madhara pale. Papa wenyewe sio lazima waende kwa maji makubwa, wanakuja pia kwa maji madogo ambapo wanatatiza wavuvi kwa kupindua dau zao. Kwa hivyo, ni lazima watu walipwe fidia ikiwa mtu amepata madhara ama ameaga dunia kwa sababu ya wale viumbe wa baharini. Kwa hayo mengi naunga mkono Mjadala huu. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}